Mourinho: Sina tatizo na Paul Pogba, lakini hatokuwa tena nahodha wa Man United, mimi ndio mkufunzi nimechukua uamuzi huo - Mase Kaleby

Breaking

Home Top Ad

Wednesday, 26 September 2018

Mourinho: Sina tatizo na Paul Pogba, lakini hatokuwa tena nahodha wa Man United, mimi ndio mkufunzi nimechukua uamuzi huo


Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa hana tatizo na kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba licha ya kumwambia mchezaji huyo kwamba hatowahi tena kuwa nahodha wa klabu hiyo.


Mourinho alimwambia Pogba kwamba sio nahodha wa klabu hiyo kutokana na wasiwasi kuhusu tabia yake.

''Ukweli ni kwamba nimechukua uamuzi huo ili asiwe nahodha wa pili lakini hakuna tatizo lolote kati yetu'', alisema Mourinho.

''Mimi ndio meneja ninaweza kufanya maamuzi kama hayo''.

Akizungumza na chombo cha habari cha Sky Sports aliongezea: Hakuna tofauti zozote kati yetu ni uamuzi tu ambao sio lazima nieleze.



Mshindi wa kombe la dunia Pogba 25 aliambiwa kuhusu uamuzi huo kabla ya mechi ya siku ya Jumanne ya kombe la Carabao dhidi ya Derby.


Mourinho amejaribu kuonyesha uzito wake baada ya kosa la Pogba kuisaidia timu ya Wolves kufunga bao la kusawazisha katika uwanja wa Old Trafford siku ya Jumamosi mbali na mchezaji huyo kukosoa mbinu zinazotumika.

Pogba alijaribu kupuuzilia mbali matamshi yake katika mtandao wa twitter siku ya Jumatatu. Lakini katika ripoti yake ya mechi ya Jumanne ambayo Derby ilishinda kwa njia ya penalti , Mourinho alisema kuwa hafurahishwi na baadhi ya wachezaji wake.

''Mechi dhidi ya Wolves ilikuwa funzo zuri , funzo ambalo ninarejelea kila wiki, funzo ambalo baadhi ya wachezaji hawajifunzi'', alisema.

Kila timu inayocheza dhidi ya United hucheza kufa kupona, na tunahitaji kuimarika ili kukabiliana nazo , Asilimia 95 haitoshi iwapo wengine wanatoa asilimia 101.



Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ,Pogba ambaye alitajwa katika kikosi dhidi ya Derby , alitazama kutoka eneo la mashabiki huku Ashley Young akiwa nahodha wa kikosi hicho.

Antonio Valencia ndio nahodha wa klabu hiyo.

Kabla ya mechi , Mourinho alisema: "wamepumzishwa . Nilimpumzisha Luke Shaw, Paul, Victor Lindelof, Antonio Valencia na David de Gea. Lazima nicheze na kikosi kizuri. "

Kufuatia sare ya 1-1 siku ya Jumamosi. Pogba alisema kwamba angetaka timu hiyo kushambulia mara kwa mara katika uwanja wa Old Trafford. Tuko nyumbani na tunafaa kucheza vizuri zaidi .

''Tuko hapa kushambulia'', alisema .Tunapocheza hivyo ni rahisi kwetu sisi.

Pogba amabaye alijiunga tena na United kutoka Juventus kwa dau lililovunja rekodi mwaka 2016 , alikuwa akiwachwa nje msimu uliopita na kusema kwamba hafurahii kusalia Old Trafford.



Mkufunzi wa Ufransa Didier Deschamps hivi karibuni alisema kuwa mtazamo wa Pogba kuwa mtu mbinafsi sio wa sawa na kwamba mashabiki na vyombo vya ahabri hawamuelewi.

No comments:

Post a Comment