Faida za Matufaa (apple) kiafya - Mase Kaleby

Breaking

Home Top Ad

Wednesday, 12 December 2018

Faida za Matufaa (apple) kiafya

Matufaa ni tunda maarufu na linalopendwa sehemu mbalimbali duniani. Tunda hili limejaa virutubisho vya phytonutrients ambavyo ni muhimu kwa afya bora ya mwili. Tufaa hujulikana kama apple kwa Kiingereza.

“An apple a day keeps the doctor away”  ni msemo maarufu kutokana na faida za tunda hili kwa afya ya mwili. Ingawa sio lazima ukila tofe kila siku hautaumwa, lakini utaboresha afya yako kwa kiasi kikubwa (ikiambatana na kufuata lishe bora).

Virutubisho Vilivyopo Kwenye Matufaa
Matofe yana virutubisho vifuatavyo:


  • Wanga
  • Vitamini C
  • Kambakamba (dietary fibers)
  • Vitoasumu (antioxidants phyto-nutrients) flavonoids na polyphenolics
  • Matofe hayana fati wala lehemu.



Matofe yana kiasi kidogo cha wanga, na kiasi kikubwa cha kambakamba.


  • Faida za Matufaa Kiafya Husaidia kupunguza  na kuulinda mwili dhidi ya sumu za mwili (free radicals). Matofe yana vitoasumu vingi vya flavonoids na polyphenolics.Hupunguza hatari ya kupata sarataniKampaundi za flavonoids zilizopo  ndani ya matofe husaidia kuondoa sumu kwenye mwili ambazo huchangia utokeaji wa saratani.
  • Kuimarisha Kinga Ya MwiliMatofe yana vitamini C kwa wingi ambayo husaidia kuimarisha kinga ya mwili ya vijidudu vya magonjwa.
  • Kulainisha ChooMatofe yana kambakamba nyingi ambazo hulainisha choo, hivyo hupunguza tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu.
  • Kupunguza Lehemu MwiliniTofe lina kambakamba ambzo husaidia kunguza unyonyaji wa lehemu kutoka kwenye utumbo. Hii husaidia kupunguza lehemu mwilini.
  • Ufanyaji Kazi Wa MoyoMatofe yana madini mbalimbali ikiwemo potasiamu kwa wingi ambayo husaidia ufanyaji kazi wa moyo vizuri.



Tahadhari
Baadhi ya watu wana allergy na matofe, kutokana na aina ya protini iliyo ndani ya matofe.

Ulaji wa mbegu za matofe unaweza kuhatarisha afya yako. Ukila mbegu nyingi sana, kama kikombe kimoja, inaweza kuleta sumu ya cyanide.

No comments:

Post a Comment