Polyculture ni uzalishaji wa samaki aina mbili au zaidi ndani ya bwawa moja. Kwa kawaida polyculture hutokea katika mabwawa. Samaki aina ya kambare na sato wanaweza kutumika, inashauriwa utumie aina hizi za samaki kwa sababu zinafaa na huleta mafanikio mazuri sana hasa pale mtu anapoamua kuwafuga.
Vifuatavyo ndivyo vigezo vya kuchagua samaki kwa ajili ya ufugaji:
Kiwango cha juu cha ukuaji wa aina ya samaki.
Samaki wanaohitajika kwa wingi katika masoko.
Chagua aina ya samaki ambayo wana kiwango cha juu cha ukuaji na kiwango cha chini cha vifo katika ukuaji.
Aina ambayo hawapatwi na magonjwa kwa urahisi.
Samaki ambao ni phytoplankton vorous au omnivorous.
Pia katika polyculture yapo masuala ya kuzingatia ni kama vile Chakula, Mavuno na Masoko yanahitajika kwanza kabla ya kuanza kufuga samaki wako.
No comments:
Post a Comment