Utunzaji wa Kuku wanao taga. - Mase Kaleby

Breaking

Home Top Ad

Monday, 3 December 2018

Utunzaji wa Kuku wanao taga.

UTUNZAJI WA KUKU WANAOTAGA

MAHITAJI YAO

Chakula bora cha kuku wanaotaga (layer's mash) gram 120 kwa kuku kwa siku au nusu(1/2) kwa kila kuku wanne kwa siku. Maji - wape maji safi na ya kutosha. Kinga dhidi ya magonjwa kama vile kideri na gumboro kila baada ya miezi mitatu. Usafi wa banda kwa
kuondoa buibui, maranda yaliyolowa, kugeuza na kusawazisha maranda kila siku.

Usafi wa vyombo vya maji na chakula. Hivi visafishwe kila siku.Kuzuia wadudu kama viroboto na chawa au kuwaangamiza kila wanapoonekana.
Kuku wasisongamane; kuku 3 - 4 katika kila meta moja ya mraba. Kuku wapewe majani ya kula ili wasidonoane.

Wawekewe viota vya kutosha, kwa wastani wa kiota kimoja cha kutagia kwa kila kuku watano. Kuku wawekewe bembea kwa ajili ya kupumzikia na kulala.

DALILI AU MUONEKANO WA KUKU ASIYETAGA

1. Kilemba kidogo, kinaonesha upungufu wa damu na kimesinyaa.
2. Huonekana kama mgonjwa.
3. Miguu yake humeremeta kwa mafuta.
4. Nafasi kati ya nyonga ni ndogo. Nafasi kati ya kifua na nyonga ni ndogo. Tumbo dogo na gumu.
5. Njia ya kutagia (Kenti) ndogo, miringo na imesinyaa.
6. Huita watoto na kuonesha hali ya kutaka kulalia mayai au kulea watoto.

UTUNZAJI WA KUKU WANAOTAGA

MAHITAJI YAO

Chakula bora cha kuku wanaotaga (layer's mash) gram 120 kwa kuku kwa siku au nusu(1/2) kwa kila kuku wanne kwa siku. Maji - wape maji safi na ya kutosha. Kinga dhidi ya magonjwa kama vile kideri na gumboro kila baada ya miezi mitatu. Usafi wa banda kwa
kuondoa buibui, maranda yaliyolowa, kugeuza na kusawazisha maranda kila siku.

Usafi wa vyombo vya maji na chakula. Hivi visafishwe kila siku.Kuzuia wadudu kama viroboto na chawa au kuwaangamiza kila wanapoonekana.
Kuku wasisongamane; kuku 3 - 4 katika kila meta moja ya mraba. Kuku wapewe majani ya kula ili wasidonoane.

 Wawekewe viota vya kutosha, kwa wastani wa kiota kimoja cha
kutagia kwa kila kuku watano. Kuku wawekewe bembea kwa ajili ya kupumzikia na kulala.

No comments:

Post a Comment