- Mase Kaleby

Breaking

Home Top Ad

Tuesday, 12 November 2019

Je ni fida gani zitokazo na juice ya Komamanga?


Komamanga ni moja ya matunda yenye ladha nzuri ambalo hupatikana katika maeneo mbalimbali duniani, lakini pia ni dawa nzuri kwa magonjwa mengi.

Asili ya tunda hilo ni Iran pamoja na Kaskazini mwa India na hufahamika kama 'Punica Granatum' kwa jina la kisayansi.

Tunda hilo hustawi kipindi cha mwezi Februari na Septemba na hustawi katika hali ya hewa ya joto. Mti wa mkomamanga pia umekuwa ukisifika kwa uwezo wake wa kuhimili hali ya hewa ya ukame.

Miongoni mwa virutubisho vinavyopatika katika komamanga ni pamoja na vitamin C, Vitamin B5, Vitamin A, Vitamin E pamoja na madini ya Potassium na ya chuma.

Uwepo wa madini ya 'potassium' na ya chuma una ashiria kuwa tunda hilo linaweza kuwafaa watu wenye matatizo ya maumivu ya viungo hasa wazee pamoja na wenye tatizo la upungufu wa damu mwilini ambapo wanashauriwa kutumia juisi ya komamanga japo glasi mbili kila siku.

Licha ya hayo komamanga pia husaidia kulinda afya ya kinywa na meno na kuzuia kuoza na kuhuisha mfumo wa kinga mwilini kwa kuondoa vijidudu na maambukizi ya virusi ndani ya mwili, halikadhalika husaidia kutibu madhaifu ya tumbo kama kuharisha na kutopata choo.

Magome ya mkomamanga pia husaidia kutoa ahueni kwa mgonjwa wa malaria au homa, hii ni pale yanapoandaliwa vizuri na kuchemshwa kisha mhusika kunywa maji yake kwa wiki mbili asubuhi na jioni kia siku.

Komamanga pia ni miongoni mwa matunda muhimu kwa afya ya wanaume kwani husaidia kulinda afya ya kibofu na moyo.

Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa komamanga lina uwezo wa kupunguza kasi ya chembechembe zinazosababisha saratani ya kibofu pamoja na ile ya mapafu hasa pale inapotumika juisi ya tunda hilo.

Pia tunda hili lina nafasi ya kuzuia shinikizo la damu mwilini pamoja na mrundikano wa sumu. Matumizi ya glasi moja ya juisi ya komamanga kila siku hutosha kumpunguzia mtumiaji hatari ya kukumbwa na tatizo hilo.

Pamoja na hayo, matumizi ya mara kwa mara ya komamanga hasa juisi yake husaidia kuimarisha mfumo wa kinga ndani ya mwili, hivyo kumfanya mhusika kutozongwa na magonjwa ya mara kwa mara.

Mbali na hayo, komamanga pia ni tunda ambalo husaidia kuboresha ubora wa manii kwa wanaume, hivyo kulifanya tunda hilo kuwa lenye nafasi ya kumwondolea mwanaume changamoto ya matatizo ya uzazi.

Komamanga pia husaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa jinsia zote mbili hii ni kutokana na kuwa na kirutubisho kiichwacho 'antioxidants' ambacho husaidia kuboresha mzunguko wa damu mwilini.

Tunda hilo pia hutumika kama huduma ya kwanza ya kukabiliana na tatizo hilo la kutokwa na damu za hedhi kwa muda mrefu. Unachopaswa kufanya ni kuandaa juisi ya tunda hilo halafu mwenye tatizo atapaswa kunywa glasi moja asubuhi wakati wa kifungua kinywa.

Anza mchakato huu kwa siku tatu kabla ya muda wa hedhi, ikiwa tayari unalijua tatizo lako na endapo lilishatokea siku za nyuma. Endelea na tiba hiyo hadi siku mbili mbele mara baada ya damu kuacha kutoka.

No comments:

Post a Comment