SINGIDA UNITED: Uongozi wa klabu ya Singida United umekiri kuyumba kiuchumi baada ya kuondoka kwa baadhi ya wadhamini ambao walikuwa wakiidhamini klabu hiyo pindi ilipopanda ligi kuu msimu wa mwaka 2017/18.
Pia uongozi huo umesema kuwa wanapata wakati mgumu wa kujiendesha kwa sasa kutokana na kukosekana kwa mdhamini mkuu wa Ligi Kuu Tanzania Bara mpaka hivi sasa.
No comments:
Post a Comment