Mara nyengine soka haieleweki
Na tuzo za soka za mchezaji bora duniani zimedhihirisha hilo.
Ni vigumu kujua utaanzia wapi, lakini tutachanganua kile kilichofanyika katika tuzo hizo zilizotiliwa shaka
Ni nini kilichokua kikifanyika katika kura ya tuzo hizo? Je kuna mtu anayeelewa kilichofanyika?
Je kikosi cha wachezaji 11 kilichochaguliwa na Fifa ndio bora zaidi duniani?
Tuanzie na mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah. Alifunga magoli 32 katika ligi ya Uingereza msimu uliopita na alitajwa kuwa mchezaji wa tatu bora wa Fifa upande wa wanaume akiwa nyuma ya Modric na Cristiano Ronaldo.Basi ni kwa nini hakuorodheshwa katika kikosi cha kwanza cha wachezaji bora 11 wa Fifa?
Halafu kuna kuorodheshwa kwa kipa wa Man United David de Gea licha ya kutoshinda taji la kipa bora lililopewa Thibaut Courtois.
Na ni vipi beki wa kulia wa Paris St-Germain anayeuguza jeraha Dani Alves aliorodheshwa miongoni mwa wachezaji 11 bora duniani wa fifa?
'Huenda Sanchez akaondoka Man Utd'
Raia huyo wa Brazil alikuwa ameorodheshwa katika timu nane kati ya tisa akikosa kuorodheshwa mwaka 2014 pekee.
Je hakuna mabeki wengine wa kulia katika timu nyengine? jamani kuna yeyote?
Ni kweli kwamba kuna shaka miongoni mwa mashabiki wa kandanda kuhusiana na kuorodheshwa kwa baadhi ya wachezaji katika kikosi hicho cha Fifa cha wachezaji 11 wa kwanza, lakini kile ambacho tuzo hizo hazitegemei ni kuwa na msimamo.
Fifa imeelezea vile kura hiyo ya kumchagua kocha bora na mchezaji bora zilivyofanyika - manahodha wa timu za taifa , wakufunzi wa timu za taifa , baadhi ya waandishi na kwa mara ya kwanza kura ya mashabiki iliopigwa katika mtandao huku kila moja ikiwa na asilimia 25.
Lakini Fifa haijaelezea ni kwa nini Salah na Courtois wanaweza kuorodheshwa katika kikosi cha pili cha wachezaji 11 bora wa Fifa mwaka huu.
Fifpro - Muungano wa wachezaji wa soka - ulitangaza vikosi vya wachezaji wa ziada wapatao 44 ambao hawakupokea kura za kutosha ili kuorodheshwa katika kikosi cha kwanza
Matokeo yake yanafurahisha
Kwa kweli washambuliaji watatu wa kikosi cha wachezaji 11 cha pili cha fIfa kinachowaorodhesha Neymar, Mohamed Salah na mshindi wa tuzo ya mchezaji aliyefunga mabao mengi katika kombe la dunia Harry Kane wanaweza kuorodheshwa vizuri katika kikosi cha wachezaji 11 bora kilichoteuliwa na Fifa
Licha ya Kane kujipatia 0.98% ya kura
Je kiungo wa kati Paul Pogba aliyeorodheshwa katika kikosi cha pili cha wachezaji 11 cha Fifa ambaye alikuwa kiungo muhimu katika ushindi wa Ufaransa, alifaa kuorodheshwa mbele zaidi ya Messi ambaye hakuwaridhisha mashabiki mbali na taifa lake kuondolewa katika mechi za makundi?
Je Kevin De Bruyne? Kiungo huyo wa Manchester City alikuwa na msimu mzuri ambao ulisaidia timu hiyo kushinda taji la ligi ya Uingereza lakini hakushirikishwa katika kikosi cha kwanza cha wachezaji 11 walioteuliwa na Fifa.
Yeye na mchezaji mwenza Kylie Walker walikuwa wachezaji pekee kutoka ManCity kuorodheshwa katika kikosi cha pili cha Fifa.
Kikosi cha tatu cha wachezaji 11 walioteuliwa na Fifa kina wachezaji wazuri walioshiriki katika kombe la dunia akiwemo mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku na kiungo wa kati wa Croatia Ivan Rakitic.
Tuambie unaonaje?
Na je bao la Salah ndilo lililokuwa bora zaidi?
Swali kuu ni bao la Mo Salah lililoshinda tuzo ya bao bora katika mechi dhidi ya Everton. Cha kushangaza zaidi ni kwamba bao hilo lilipata asilimia 38 ya kura ilioipigwa na raia.Ni kweli kwamba ni juhudi nzuri kutoka kwa raia huyo wa Misri, lakini je bao hilo lilikuwa bora zaidi ya lile la Gareth Bale alilofunga wakati wa mechi ya vilabu bingwa dhidi ya Liverpool?
Bao hilo halikushinda hata bao bora la ligi mnamo mwezi Disemba 2017, lakini ni bao la Jermain Defoe lililoibuka mshindi dhidi ya Crystal Palace mwezi huo.
Mashabiki walipigia kura bao la Salah kuwa bao bora miongoni mwa mabao kumi yalioorodheshwa, ikiorodhesha bao la Benjamin Pavard wa Ufaransa katika kombe la dunia ,bao la Mreno Ricardo Quaresma dhidi ya Iran na bao la Cristiano Ronaldo alipokuwa akiichezea Real Madrid dhidi ya Juventus katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.
Mchezaji mwenza wa Salah katika timu ya Liverpool James Milner alituma ujumbe wa twitter akifurahia tuzo hiyo ya Salah.
No comments:
Post a Comment