RAIS mstaafu wa Brazil, Bw. Michel Temer, ametiwa mbaroni jijini Sao Paulo kwa tuhuma za rushwa na ufisadi.
Mstaafu huyo alitiwa mbaroni baada ya kinga aliyokuwa nayo ya kutoweza kushtakiwa akiwa madarakani kumalizika. Temer alikuwa rais tangu mwaka 2016 mpaka 2018.
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 78 ambaye kitaaluma ni mwanasheria, mara baada ya kuondoka madarakani, Ofisi za Mwendesha Mashitaka wa Serikali zilianza uchunguzi wa tuhuma za magendo, rushwa na ufisadi dhidi yake.
Oparesheni ‘Car Wash’ ni jina rasmi la oparesheni dhidi ya viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara na watumishi wa umma wanaotuhumiwa kwa ufisadi nchini Brazil ili kusafisha na kutokomeza ufisadi na rushwa. Pamoja na ufisadi, Temer anatuhumiwa kwa ufisadi katika mradi mkubwa wa kuzalisha nguvu za umeme katika jimbo la Rio de Janeiro na katika sekta ya madini.
Marais wastaafu wawili waliopita wa Brazil pia wamekumbwa na operesheni Car Wash kutokana na matumizi mabaya ya madaraka wakiwa ofisini na hivyo kutuhumiwa kuendekeza ufisadi na rushwa.
No comments:
Post a Comment